WANAFUNZI WA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KUFURAHIA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA SEKTA YA ELIMU VYUO VYA KATI
Prof. Carolyne Nombo amekutana na Balozi wa Poland Nchini Tanzania kujadili kuhusu kukuza ushirikiano katika sekta ya Elimu
Karibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Mei 17 2024 amekutana na Balozi wa Poland Nchini Tanzania Mhe. Krzystof Buzalski ambapo wamezungumzia kuhusu kuendelea kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya Elimu.
Prof. Carolyne Nombo amezindua Alama ya kipekee inayoelekeza kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Mei 17, 2024 amezindua Alama ya kipekee inayoelekeza kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika eneo la Barabara ha Sam Nujoma.
Prof. Adolf Mkenda ameshiriki Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Elimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola
Mhe. Prof. Adolf Mkenda (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ameshiriki Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Elimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Marlborougj House, London, Uingereza kuanzia tarehe 16 hadi 17 Mei 2024.
Prof. Carolyne Nombo amekutana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa kujadiliana na masuala mbalimbali ya Elimu
Karibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Mei 16, 2024 amekutana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Canada Mhe. Ahmed Hussen kujadiliana na masuala mbalimbali ya Elimu.

Prof. Nombo ameishukuru Serikali ya Nchi hiyo kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP).
Kongole Mhe. Dkt. Mpango
Picha mbalimbali za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akinunua vitabu katika maduka jijini Dar es salaam ikiwemo Duka la Mkuki na Nyota na Pauline’s Bookshop.

Makamu wa Rais hutumia muda wa mapumziko katika kujisomea vitabu kwa lengo la kuongeza maarifa katika njanja mbalimbali za uchumi, utawala, dini, siasa, kilimo na ufugaji vilivyoandikwa na waandishi wa ndani na nje ya nchi.
Prof. Nombo Aridhishwa na Kazi - Ujenzi wa VETA Wilaya ya Muheza
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameridhishwa na kazi inayoendelea ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA cha Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Prof. Nombo akikagua ujenzi wa Chuo hicho Mei 15, 2024 amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na kushirikiana kikamilifu na Msimamizi wa mradi huo ili kukamilisha kwa wakati.

