Prof. Mkenda ameitaka TCU kuendelea kushirikiana na Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika mchakato wa kufanya maboresho ya mitaala

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuendelea kushirikiana na Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika mchakato wa kufanya maboresho ya mitaala ili iendane na Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala Mipya ya Elimu Msingi

Swahili

Serikali imesimamia mifumo ya ajira na ajira zote za kudumu ziko chini ya Serikali Kuu ikiwemo na za sekta ya elimu kwa walimu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wafanye mapitio ya ikama zao kuangalia mlundikano wa walimu katika maeneo ya mijini na pembezoni mwa barabara na kuwasambaza katika maeneo ya vijijini ili kuwe na utoshelevu wa walimu katika maeneo yao.

Swahili

Rais Samia Atunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima Korea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr wa kwanza kulia, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03 June, 2024. Wa kwanza kushoto ni Amidi wa Shule Kuu Soo Chang Hwang

Swahili

Tunawashukuru kwa kushiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024

Tunamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Gilbert Kalima wa kwanza kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Japhari Kubecha, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Zainabu Abdallah na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Hashim Mgandilwa kwa kushiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 jijini Tanga

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS