bunifu katika Maoesho ya mwaka huu zimejikita katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii - Mhe. Husna Sekiboko

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni Mhe. Husna Sekiboko amesema bunifu katika Maoesho ya mwaka huu zimejikita katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii.



Mhe. Sekiboko amesema hayo Mei 31, 2024, jijini Tanga wakati akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.

Swahili

Ubunifu wa Teknolojia mbalimbali zilizojipambanua katika Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni kielelezo cha Uwekezaji wa Miundombinu ya kielimu - Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amesema matokeo ya ubunifu wa Teknolojia mbalimbali zilizojipambanua katika Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni kielelezo tosha cha uwekezaji wa miundombinu ya kielimu ambayo imewekezwa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Swahili

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili jijini Tanga

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili jijini Tanga kuhitimisha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal.

Swahili

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa awasili Jijini Tanga kuhitimisha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa awasili jijini Tanga kuhitimisha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal.



Kauli Mbiu yetu: Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi Shindani.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda na Viongozi mbalimbali wawasili tayari kwa mapokezi ya Waziri Mkuu kushiriki Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni Mhe. Husna Sekiboko, Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mhe. Hamis Taletale na Mkuu wa wilaya Pangani Mhe. Zainabu Abdullah wawasili tayari kwa mapokezi ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kushiriki Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 jijini Tanga.

Swahili

kuanzia Mwaka huu hakutakuwa na maswali ya kuchagua katika mitihani ya Hisabati - Dkt. Said Mohamed

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) Dkt. Said Mohamed amesema kuwa kuanzia Mwaka huu hakutakuwa na maswali ya kuchagua katika mitihani ya Hisabati.

Akiwasilisha taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi Mei 30, 2024 Jijini Tanga Dkt. Mohamed amesema kuwa tayari mafunzo yameshatolewa kwa ajili ya kutekeleza hilo huku akihimiza ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali.

Swahili

Serikali Kuweka Mikakati ya Kupima Ubora wa Elimu Nchini

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali inaweka mikakati ya kuendelea kupima ubora wa elimu kwa kuzingatia vigezo Kitaifa na Kimataifa.

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Mei 30, 2024 jijini Tanga wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya Tathimini ya ujifunzaji na ufaulu wa Wanafunzi ambapo amesema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kuongeza ubora wa elimu na kwamba suala muhimu ni kujipima Kitaifa na Kimataifa.

Swahili

Prof Nombo na wadau mbalimbali wa elimu Wamewasili katika hafla ya Uwasilishwaji wa Taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi

Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo na wadau mbalimbali wa elimu tayari wamewasili katika hafla ya Uwasilishwaji wa Taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi inayofanyika Jijini Tanga.

Swahili

Mhe. Omari Kipanga Ameishukuru Serikali ya marekani kupitia Ubalozi wake hapa nchini kwa kudhamini kituo cha kisasa cha TEHAMA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga Ameishukuru Serikali ya marekani kupitia ubalozi wake hapa nchini kwa kudhamini kituo cha kisasa cha Tehama katika Maktaba ya Dodoma kitakachotumika na watanzania kupata maarifa na stadi mbalimbali zitakazo wawezesha kutimiza ndoto zao

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS