MOEST yawakutanisha Wadau wa Elimu kujadili Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia katika Elimu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yawakutanisha wadau wa elimu, sayansi na teknolojia kujadili Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia katika Elimu.



Mkutano huo wa siku mbili unaoanza leo Juni 24 hadi 25, 2024 utafunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Carolyne Nombo jijini Dar es Salaam.

Swahili

Mawaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kushiriki Mkutano wa kisekta wa 19 wa EAC

Mawaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana Juni 22, 2024 jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa kisekta wa 19 wa EAC

Swahili

Prof. Carolyne Nombo Ametembelea Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) Kampasi ya Kikuletwa

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Juni 21, 2024 Jijini Arusha ametembelea Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) Kampasi ya Kikuletwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo mapya ya Chuo hicho yatakayotumika kutoa mafunzo ya uzalishaji wa Nishati Jadidifu (Renewable Energy) yanayojengwa na Wizara kupitia Mradi wa Afrika Mashariki wa kujenga ujuzi kwa mlingano na uingiliano wa kikanda (EASTRIP)

Swahili

ASANTENi

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawashukuru wadau wote wa habari kwa ushirikiano na kuwezesha kupata nafasi ya Sita katika utoaji habari na taarifa na Elimu kwa Umma kati katika Kundi la Wizara.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi Sylvia Lupembe akipokea Cheti cha ushindi huo kutoka kwa Mhe Nape Nnauye(Mb) Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda Amekutana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kujadili namna mbalimbali za kuboresha Elimu Nchini

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ally Abdulgulam Hussein leo Juni 21, 2024 wametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutaka Wizara hizo zikutane kujadili namna mbalimbali za kuboresha Elimu Nchini.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda wamekutana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Jijini Dodoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ally Abdulgulam Hussein leo Juni 21, 2024 wamekutanaJijini Dodoma na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya Elimu na ushirikiano katika kutekeleza mageuzi katika sekta hiyo hususan Sera na Mitaala iliyoboreshwa.

Swahili

Vyombo vya Habari ni Mshirika muhimu katika kufikia malengo ya Taasisi za umma

Vyombo vya Habari ni Mshirika muhimu katika kufikia malengo ya Taasisi za umma katika uhabarishaji na elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na Kiuchumi.



Hayo yameelezwa leo Juni 19, 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Sylvia Lupembe wakati akichangia mjadala kuhusu namna ya kutumia Mawasiliano kimkakati kuleta Maendeleo.

Swahili

Kongamano la Kwanza, Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Lazinduliwa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM

Kongamano la kwanza lenye dhamira ya kujadili maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia Uvumbuzi yanavyoweza kuchangia maendeleo endelevu katika viwanda na jamii.



‘Vyuo vikuu vimefanya kazi ya kufanya tafiti na kutangaza matokeo ya tafiti hizo yanayosaidia katika usuluhisho wa changamoto za kijamii.’ Amesema hayo Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula akifungua kongamano hilo.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS