Mshindi wa Pili wa Shindano la Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza

Sophia Mosses Kawegere kutoka Shule ya Msingi Enaboishu iliyopo Wilayani Arusha. Mkoani Arusha akipokea zawadi kutoka kwa Prof. Carolyne Nombo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia baada ya kuibuka Mshindi wa Pili



Zawadi hiyo imekabidhiwa Juni 25, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwatambua walimu katika Mashindano ya Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi.

Swahili

Serikali inaendelea na Kazi ya Kuboresha Miundombinu na Kuweka Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema serikali itaendelea na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu na kuweka vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika Shule.



Prof. Mkenda amesema hayo Juni 25, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la stadi za kufundisha somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi kwa Tanzania Bara.

Swahili

Katika Mitaala iliyoboreshwa Ufundishaji wa Masomo ya Lugha Umeboreshwa

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa katika mitaala iliyoboreshwa ufundishaji wa masomo ya lugha umeboreshwa.



Prof. Nombo amesema hayo Juni 25, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la stadi za kufundisha somo la Kingereza kwa Shule za Msingi.

Swahili

Shindano la Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi limeshirikisha shule za Umma katika Halmashauri zote za Tanzania Bara

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba amesema kuwa shindano la Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi limeshirikisha shule za Msingi za Umma katika Halmashauri zote za Tanzania Bara.



Dkt. Komba ameongeza kuwa jumla ya walimu 3705 wameshiriki katika shindano hili ambapo katika mchujo wamepatika walimu 10 ambao kazi zao zitarekodiwa na studio za TET na kuwekwa katika Maktaba Mtandao ya Taasisi hiyo.

Swahili

WyEST kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) itatoa Tuzo kwa Walimu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) itatoa Tuzo kwa Walimu walioshinda Shindano la Pili la Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi.



Halfa ya utoaji Tuzo hizo inafanyika leo Juni 25, 2024 Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda atakabidhi Tuzo hizo kwa washindi.

Swahili

Jadilini namna bora ya Kuratibu na Kufungamanisha juhudi za Wadau wa Elimu Nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ametoa wito kwa wadau wanaojadili Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia za Kijiditali katika Elimu pamoja na mambo mengi kujadili namna bora ya kuratibu na kufungamanisha juhudi za wadau mbalimbali katika eneo hio nchini.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS