Prof. Carolyne Nombo Anafungua Kongamano la 12 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Juni 27, 2024 anafungua Kongamano la 12 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), ambalo pia ni maalumu kwa ajili ya kumuenzi Mkuu wa Kwanza wa Chuo Kikuu hicho na Rais wa Pili wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Swahili

Norway Kuendelea Kushirikiana na Tanzania Kieleimu

Wadau wa Elimu kutoka nchini Norway wamekutana na kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula juu ya ushirikiano wa masuala ya Elimu ya Juu, Utafiti na mabadiliko ya tabia nchi.



Dkt. Rwezimula amesema Watanzania wengi wanaendelea kunufaika na ushirikiano huu ikiwa ni pamoja na kupata ufadhili wa masomo ya Elimu ya Juu nchini Norway, pamoja na unanzishwaji wa miradi 18 na Taasisi 9 nchini kutoka kwenye programu ya NORHED.

Swahili

Nafasi ya Tatu katika Mashindano ya Walimu Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza

Nafasi ya Tatu katika mashindano ya walimu Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi imechukuliwa na Mwalimu Jenester Paulo Mmasi kutoka Shule ya Msingi Tuvaila iliyopo katika Halmashauri ya Meru Mkoani Arusha. akipokea zawadi kutoka kwa Mwakalishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Perri Arora

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS