ENABEL Wapokea Tuzo ya Shukrani Kuendeleza Ushirikiano Utekelezaji Miradi ya Elimu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 03, 2024 inetoa Tuzo ya Shukrani kwa Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABEL) kwa kudhamini Wiki ya Elimu Ujuzi na Ubunifu Mwaka 2024 iliyofanyika Mkoani Tanga Mwezi Mei.

Tuzo hiyo imekabidhiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Profesa Carolyne Nombo ambae amewashukuru kwa ufadhili huo pamoja na ufadhili miradi ya elimu Mkoani Kigoma.





