Wizara ya Elimu Kushirikiana na Taasisi ya Vignans ya India eneo la Sayansi, Teknolojia na Utafiti
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imetia saini makubaliano ya ushikirikiano na Taasisi ya Utafiti, Sayansi na Teknolojia ya Vignan's kutoka India.

Makubaliano hayo ni katika masuala ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Utafiti ikiwa ni pamoja na taasisi hiyo kupokea wanafunzi 100 kutoka Tanzania kila mwaka kwa ajili ya kusoma fani za kipaumbele ikiwemo Uhandisi ujenzi, Uhandisi Kilimo, Akili Mnemba, na Uhandisi wa Umeme kwa gharama nafuu.





