OMBWE NI KARAKANA YA SHETANI
Michezo Itasaidia Vijana Kujiepusha na Matendo Maovu
Imeelezwa serikali kuwa itahakikisha michezo inaendelezwa shuleni kwa sababu inasaidia vijana kujiepusha na matendo yasiyofaa.

Hayo yamesemwa leo Julai 20, 2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu ya Wazazi Dar es salaam Super Cup yaliyoanza kutimua vumbi rasmi katika viwanja vya Bandari Jijini Dar es salaam,
DKT RWEZIMULA AWAITA WANANCHI KUJIUNGA VETA NJOMBE
Prof. Carolyne Nombo na Wataalamu wa Elimu Wameshiri Kikao cha Pamoja na Wizara Ya ElimuMsingi ya Afrika Kusini
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo na wataalamu wa elimu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameshiriki kikao cha pamoja na Wizara Ya ElimuMsingi ya Afrika Kusini ambapo ameipongeza Wizara hiyo kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika sekta ya elimu.
VETA Njombe Kuanza kutoa Mafunzo
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wameagizwa kuhakikisha Chuo cha VETA cha Mkoa wa Njombe kinapelekewa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kianze kutoa mafunzo kwa wakazi wa mkoa huo.
Kuweni Wabunifu Kutekeleza Majukumu ili kuwapatia Vijana wa Mkoa wa Njombe Elimu na Ujuzi
Watumishi wa Chuo cha Wananchi Njombe (FDC) wametakiwa kiwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ili kuwapatia vijana wa Mkoa wa Njombe elimu na ujuzi utakaowasaidia kujianiri ama kuajiriwa.

Wito huo umetolewa Julai 19, 2024 Mkoani Njombe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezamula wakati alipofika mkoani humo kufatilia mradi wa ukarabati wa chuo hicho.
Timu ya Benki ya Dunia imetembelea Chuo Kikuu cha MUST kukagua maendeleo ya Mradi HEET
Timu ya Benki ya Dunia imetembelea Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia, Mbeya kukagua maendeleo ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaojenga miundombinu chuoni
Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Dar es Salaam Kampasi ya Myunga Songwe
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Dar es Salaam Kampasi ya Myunga Songwe

Prof. Mkenda amefanya ziara hiyo na kukagua miundombinu ya kampasi hiyo akiwa ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezamula.
Lugha ya Kiswahili Yaendelea Kuchanja Mbuga
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo anaendelea na ziara ya mafunzo nchini Afrika Kusini akiwa anaongoza timu ya wataalam kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanaoshughulika na Sayansi, Teknolojia na ElimuMsingi.

Ziara hiyo pia ni sehemu ya utekelezaji wa hati ya Makubaliano baina ya Tanzania na Afrika Kusini kuhusu kuhusu ElimuMsingi ikiwemo ufundishaji wa Kiswahili katika shule za Afrika Kusini.

