Prof. Adolf Mkenda ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Kampasi ya Kikuletwa

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 30, 2024 ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Kampasi ya Kikuletwa itakayokuwa Kituo cha Umahiri cha Nishati Jadidifu.



Kampasi hiyo inajengwa katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuzalisha wataalamu wa Nishati Jadidifu wasiopungua 1,500 kwa Mwaka.

Swahili

Wataalam wa Nishati Jadidifu Kupikwa Kikuletwa Wilayani Hai

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa Mradi wa Kujenga na Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki (EASTRIP) ni muhimu kwa kuwa una kwenda kusaidia katika utekelezaji wa mabadiliko ya kielimu ambayo yameaanza kutekelezwa kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023 pamoja na Mitaala mipya katika ngazi mbalimbali.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo, Amewasili Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro

Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Julai 30, 2024 amewasili Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kushuhudia uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Kampasi ya Kikuletwa.



Kampasi hiyo inajengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EASTRIP) inatarajiwa kuwa Kituo cha Umahiri cha kutoa Wataalam wa Nishati Jadidifu

Swahili

Ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu kwa Shahada za Umahiri (MSc) katika Fani za Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imetangaza kutoa ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu nje ya nchi kwa asilimia miamoja kwa shahada za umahiri (MSc) katika fani za sayansi na teknolojia ya nyuklia.



Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri katika Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda amesema Mwaka huu wa Fedha 2024/2025 Samia Scholarship Extended imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 1.6 kuwezesha mpango huo.

Swahili

Shule za Msingi za Serikali 854 zenye Wanafunzi 437,749 sawa na asilimia 70 ya Wanafunzi zimeweza kutoa Huduma ya Chakula Shuleni

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2024, Shule za Msingi za Serikali 854 zenye Wanafunzi 437,749 sawa na asilimia 70 ya Wanafunzi zimeweza kutoa huduma ya chakula Shuleni.



Aidha ameongeza kuwa Shule za Sekondari za Serikali 261 zimetoa chakula kwa Wanafunzi 143,700 sawa na asilimia 69.2 na kwamba Mkoa walau umepiga hatua japo juhudi zaidi zinaendelea kutekelezwa.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo Ametembelea Maonesho katika Kongamano la Utoaji wa Chakula na Lishe Shuleni

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Julai 26, 2024 ametembelea maonesho katika Kongamano la Utoaji wa Chakula na Lishe Shuleni linalofanyika Viwanja vya Morena Hotel Jijini Dodoma.



Kauli Mbiu: Huduma ya chakula na lishe kwa afya na elimu bora.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS