Ni Muhimu Kuzingatia Suala la Chakula na Lishe Bora kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum

Mkurugenzi wa Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Magreth Matonya amesema ni muhimu kuzingatia suala la chakula na lishe bora kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum, kwa sababu baadhi yao wanapata madhara ya kiafya kutokana na kukosa huduma bora.



Dkt. Matonya amesema hayo Julai 25, 2024 wakati akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Utoaji Chakula na Lishe Shuleni linalofanyika jijini Dodoma.

Swahili

Bi. Abigail Marwa Ameipongeza WyEST kuwa Miongoni mwa Wizara Zinazochangia na Kusimamia Kikamilifu Suala la Chakula na Lishe Shuleni.

Mratibu wa Masula ya Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Abigail Marwa ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwa miongoni mwa Wizara mtambuka zinazochangia na kusimamia kikamilifu suala la chakula na lishe Shuleni.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo Amekutana na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF)

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Julai 24,2024 Jijini Dodoma amekutana na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bw. Daniel Baheta na kufanya mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano katika sekta ya elimu.

Swahili

Prof Mkenda amemshukuru Baheta kwa kushirikiana na Wizara katika kutekeleza Miradi na mipango ya Sekta ya Elimu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula leo Julai 23, 2024 Jijini Dodoma wamekutana na kumuaga Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) Bw. Daniel Baheta anayetarajia kuondoka nchini Tanzania mwishoni mwa Mwezi Agosti baada ya kupata uhamisho wa kikazi kuelekea nchini Sudani.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS