Waandishi wa Vitabu Waomba Uhamasishaji Usomaji

Mwandishi wa Kitabu cha *Tangled Web* Euanice Urio ameiomba Serikali kusaidia katika mnyororo wa Sekta ya Uandishi wa Vitabu ili kuwezesha upatikanaji wa vitabu na kuhamasisha usomaji nchini



Akizungumza Agosti 02, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kitabu chake hicho, Urio amesema kuwa changamoto kubwa katika sekta hiyo ni kuvipeleka sokoni kutokana na watanzania wengi kutokuwa na tabia ya usomaji wa vitabu.

Swahili

Waandishi wa Vitabu waitwa TET kupata Ithibati Vitumike katika Shule

Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amewataka waandishi wa vitabu nchini kuviwasilisha TET ili vipatiwe ithibati kwa ajili ya kutumika shule.



Dkt. Komba amesema hayo Agosti 02, 2024 Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kitabu cha Mwandishi Euanice Urio kiitwacho *Tangled Web* ambapo amesema utaratibu wa kupeleka vitabu TET ni wa kawaida ili kuona kama vina maudhui yanayoweza kutumika shuleni na kuwajenga watanzania.

Swahili

Serikali yatenga Fedha kununua Vitabu vya Maktaba Nchini

Serikali imetenga fedha katika Bodi ya Maktaba Tanzania kwa ajili ya ununuzi wa vitabu ili kuwezesha watanzania kupata vitabu na kujenga tabia ya usomaji.



Hayo yameelezwa Agosti 02, 2024 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha Riwaya chenye jina *Tangled Web* kilichoandikwa na Euanice Urio.

Swahili

Dkt. Leonard Akwilapo akipokea vitendea kazi tayari kuongoza timu ya Bodi kutoka kwa Prof. Adolf Mkenda

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Leonard Akwilapo akipokea vitendea kazi tayari kuongoza timu ya Bodi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.



Dkt. Akwilapo amekabidhiwa vitendea kazi hivyo Agosti 02, 2024 katika Hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za ADEM Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo ameipongeza Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameipongeza Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) iliyomaliza muda kwa kufanya kazi ya kuishauri wizara juu ya usimamizi na uendeshaji wa Wakala kwa kuzingatia malengo yakekatika kutekeleza majukumu.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo amewasili Wilayani Bagamoyo tayari kushuhudia Uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya ADEM

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amewasili wilayani Bagamoyo tayari kushuhudia uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).



Bodi hiyo iliyoteulewa hivi karibuni inatarajiwa kuzunduliwa Agosti 02, 2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda

Swahili

Prof. Adolf Mkenda atembelea Chuo cha Ufundi cha Kibosho

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 31, 2024 alitembelea Chuo cha Ufundi cha Kibosho kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.



Akiwa Chuoni hapo alipata nafasi ya kukagua karakana na miradi mbalimbali ya chuo ikiwemo ufugaji wa ng'ombe, Kuku, Mbuzi, Nguruwe pamoja na shamba la chuo.
Miradi hiyo yote inatoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi.

Swahili

Prof Mkenda anafungua Kongamano la nne la Kimataifa la Ushirika linalofanyika Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Julai 31, 2024 anafungua Kongamano la nne la Kimataifa la Ushirika linalofanyika Mkoani Kilimanjaro.



Kongamano hilo la siku tatu limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na Chuo Kikuu cha Ushirika cha Kenya, kauli mbiu ya kongamano hili ni *Ushirika kwa Maendeleo Endelevu*

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS