Shangwe la RC Sendiga akipokea Wanafunzi Shule ya Wasichana Maisaka

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ameonesha kufurahishwa kukamilika na kuanza kwa Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Maisaka ya mchepuo wa Sayansi na kutokea Shuleni hapo akiwa amevalia sure ya shule hiyo.



Shule hiyo ni miongoni mwa Shule 26 zilizojengwa na Mradi wa Kuboresha Elimu ya sekondari (SEQUIP) unaotekelezwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Swahili

Prof. Nombo ameshiriki Programu ya Ushirikiano wa Mabadilishano katika Mageuzi ya Elimu kwa nchi za Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS)

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Agosti 13, 2024 ameshiriki Programu ya Ushirikiano wa Mabadilishano katika Mageuzi ya Elimu kwa nchi za Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Afrika Mashariki (EAC).



Program hii inalenga kuwezesha Nchi Wanachama wa ECOWAS na EAC kutekeleza mahusiano katika Elimu Msingi, Ubora wa Usawa unaojumuisha Jinsia na Elimu ya Kidigitali.

Swahili

Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya Elimu kutoka na mabadiliko ya  Sera na mitaala ya Elimu pamoja na maboresho ya miundombinu ya elimu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya Elimu kutoka na mabadiliko ya  Sera na mitaala ya Elimu pamoja na maboresho ya miundombinu ya elimu.

Swahili

Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango akisalimiana na Prof. Adolf Mkenda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Kwenye Mkutano wa Elimu wa Kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sherehe za Mwaka wa Elimu wa Umoja wa Afrika 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Swahili

Mkutano wa Elimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kuendelea leo Arusha

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo wamewasili katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha kushiriki ufunguzi wa Mkutano wa Elimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza jana Agosti 12, 2024.



Mkutano huo unashirikisha nchi zote za Afrika Mashariki na unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango.

Swahili

Prof. Nombo amekutana na wadau wa elimu kutoka ADEA kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa Ukusanyaji wa Takwimu za Elimu na Ustadi.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Agosti 12, 2024 Jijini Dodoma amekutana na wadau wa elimu kutoka Chama cha Maendeleo ya Elimu barani Afrika (ADEA) kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa Ukusanyaji wa Takwimu za Elimu na Ustadi.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS