Prof. Carolyne Nombo akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa katika Viwanja vya Mzazi Moja Ikulu Zanzibar katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliopata daraja la Kwanza (Division One) katika Mtihani wa Kidato cha Nne na Sita.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Wanafunzi katika Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Wanafunzi katika Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar kabla ya kuanza hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliopata daraja la Kwanza (Division One) katika Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2023 na Sita Mwaka 2024.



Wanafunzi hao wametumia fursa hiyo kumuelezea nia na malengo yao katika kuendelea na masomo yao Elimu ya Juu

 

Swahili

Prof. Carolyne Nombo amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Agosti 26, 2024 amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said kuona namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara hizo mbili katika masuala ya Elimu ikiwemo Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.



Katika mazungumzo hayo Prof. Nombo ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Teknolojia Prof. Ladislaus Mnyone.

Swahili

KIZIMKAZI IMEITIKA

Kizimkazi imeitika Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo katika kilele cha Kizimkazi Festival 2024 sambamba na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdulla Said.



Katika Tamasha hilo Miradi kadhaa ya Elimu imezinduliwa ikiwemo Samia Academy maalum kwa amali ya michezo, Skuli ya Sekondari Kizimkazi Dimbani na Dahalia ya Wasichana katika shule hiyo.

Swahili

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imegharamia kwa asilimia miamoja mradi wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi Dimbani

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imegharamia kwa asilimia miamoja mradi wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi Dimbani iliyopo Kisiwani Unguja kwa kutumia fedha za direct indicators, ambapo jumla ya shilingi Milioni 223 zimetumika.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS