Majaliwa Ahimiza Kuchangamkia Fursa za Mafunzo Fani za Sayansi na Teknolojia
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema, Serikali inaendelea kuweka msisitizo suala la elimu, na katika Mwaka wa fedha 2024/25 imetenga Sh. bilioni 787 kwa ajili ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Mhe. Majaliwa amesema hayo Agosti 27, 2024 akimwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 50 ya Idara ya Ujenzi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (KIST) visiwani Zanzibar.
Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Maonesho katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya KIST
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Agosti 27, 2024 ametembelea Maonesho katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Idara ya Ujenzi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (KIST) viwanja vya Golden Tulip Visiwani Zanzibar
Prof. Adolf Mkenda na Prof. Carolyne Nombo waungana na Wazanzibar kusherekea Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa KIST
Leo Agosti 27, 2024 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo waungana na Wazanzibar kusherekea Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Idara ya Ujenzi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (KIST) katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.
Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi. Lela Mohamed
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi. Lela Mohamed katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Idara ya Ujenzi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia Karume (KIST) Agosti 27, 2024 katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar.

MKENDA AKIHITIMISHA WASILISHO LA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
Rais Mwinyi Akoshwa na Mafanikio katika Sekta ya Elimu
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya Elimu kuwezesha mazingira rafiki ya ujifunzaji, kuongeza fursa za mikopo na kuzingatia maslahi bora kwa Walimu.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini zoezi la zawadi kwa Wanafunzi waliofaulu kwa kupata daraja la Kwanza katika Mtihani
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini zoezi la zawadi kwa Wanafunzi waliofaulu kwa kupata daraja la Kwanza katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2023 na Kidato cha Sita 2024 upande wa Unguja.

Halfa ya kuwapongeza Wanafunzi hao imefanyika Agosti 26, 2024 Viwanja vya Mnazi Mmoja Ikulu Zanzibar
Samia Skolashipu Inahamasisha Usomaji Fani za Sayansi - Mkenda
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema uwepo wa Samia Skolashipu imekuwa ni kivutio kuwahamasisha wanafunzi wenye uwezo mkubwa katika Sayansi kuendelea kusomea fani za Sayansi ambazo zinalenga kuchochea ustawi na maendeleo ya Taifa.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliopata daraja la Kwanza katika Mtihani yao
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi Agosti 26, 2024 ameambatana na Mama Maryam Mwinyi katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi waliopata daraja la Kwanza katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2023 na Kidato cha Sita 2024 Viwanja vya Mnazi Mmoja Ikulu Zanzibar.

