Mambo Safi Ujenzi wa Shule ya Sekondari Wasichana ya Sayansi Mkoa wa Dar es Salaam

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti Mh. Husna Juma Sekiboko imeridhiswa na ujenzi wa Shule maalum ya wasichana ya Mkoa wa Dar es salaam.



Shule hii ni moja kati ya Shule 26 za Sekondari za wasichana za Sayansi zilizojengwa nchini ili kuongeza fursa za wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi. Shule hizi zinajengwa kupitia Programu ya Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP)

Swahili

Kasi ya utekekezaji wa Mradi wa BOOST yawakosha Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo

Kasi ya utekekezaji wa Mradi wa BOOST yawakosha Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo inayongozwa na mwenyekiti wake Mh. Husna Juma Sekiboko.



Kamati hiyo iko katika ziara ya kukagua miradi hiyo ambapo leo Septemba 10 wametembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Mkondo wa Kingereza ya Richard Mgana inayojengwa na mradi kwa Shilingi za Kitanzania 475,300,000 Kigogo Jijini Dar es salaam.

Swahili

Maafisa Habari Wizara ya Elimu na Taasisi zinazotekeleza Mradi wa EASTRIP wamekutana kuweka mikakati ya pamoja

Maafisa Habari Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi zinazotekeleza Mradi wa EASTRIP (East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project)

wamekutana jijini Dar es Salaam kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha mradi unatangazwa na jamii inaufahamu.

Swahili

Mkenda akutana na Mwenyekiti wa Baraza la NACTVET Bi. Bernadetta Ndunguru

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo jijini Dodoma amekutana na  kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Bi. Bernadetta Ndunguru ambae alifika kwa ajili ya kujitambusha .

Katika kikao hicho Prof. Mkenda amesisitiza Bodi ya NACTVET  kuendelea kuimarisha na kusimamia elimu ya Ufundi katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo inayojielekeza katika elimu ujuzi. 
 

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS