Kibaha Mambo ni Moto

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na mwenyekiti wake Mh. Husna Juma Sekiboko imeendelea na ukaguzi wa miradi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inayotekelezwa nchini ambapo imeshuhudia ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Shimbo Mkuza ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP.

Swahili

Kamati ya Bunge Yaridhishwa na Ujenzi Kituo cha Taasisi ya Elimu Watu Wazimz Kibaha

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeridhishwa na kasi, ubora wa ujenzi wa majengo ya kituo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yanayojengwa
Kibaha Mkoani Pwani,



Majengo hayo yanajengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa SEQUIP ili kutoa fursa kwa wanafunzi wanaosoma nje ya mfumo rasmi wa Elimu wakiwemo walikatisha masomo kwa sababu mbalimbali kama ujauzito, na utoro na sababu nyingine kama za kiuchumi.

Swahili

Prof. Nombo ametembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu na kukagua karakana zinazotumika kutoa mafunzo kwa vitendo

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Septemba 11, 2024 ametembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu na kukagua karakana zinazotumika kutoa mafunzo kwa vitendo katika fani mbalimbali zinazofundishwa katika Chuo hicho.



Katika ziara hiyo Prof. Nombo ameambatana na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Canada Nchini Tanzania (Global Affairs Canada) Bi. Stephanie Brunet na Bi. Rasmata Barry.

Swahili

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekagua maendeleo ya ujenzi wa karakana za kufundishia wanafunzi wanaosoma Uhandisi katika Chuo cha UDSM

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekagua maendeleo ya ujenzi wa karakana za kufundishia wanafunzi wanaosoma Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zinazojengwa kupitia Mradi wawa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET)

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS