WAZIRI MKUU DKT. NCHEMBA AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA UFUNDI ROMBO – KILIMANJARO
SERIKALI YAOKOA BILIONI 6 KUPITIA MANUNUZI YA PAMOJA YA SARUJI KWA UJENZI WA VETA
WAZIRI MKENDA: TET KUIMARISHA UPATIKANAJI WA VITABU VYA KIADA NA ZIADA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof.Adolf Mkenda, amesema kuwa jukumu la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ni kuandaa na kusambaza vitabu vya shule, ikiwemo vitabu vya kiada na ziada, kwa kushirikiana na waandishi wa ndani ili kuhakikisha upatikanaji wa machapisho bora kwa wanafunzi nchini.
UZINDUZI WA VITABU VYA TUZO YA TAIFA YA UANDISHI: HATUA MPYA KUKUZA ELIMU NA VIPAJI VYA NDANI
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Anneth Komba, amesema kuwa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi bunifu ni nyenzo muhimu ya kuibua na kukuza vipaji vya waandishi wa ndani.
PROF. MLAMA: WAANDISHI 31 WASHIRIKI TUZO YA TAIFA YA UANDISHI
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere, Prof. Penina Mlama, amesema kuwa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu imeongezeka kutoka nyanja mbili za awali riwaya na ushairi hadi kufikia nyanja nne ambazo ni riwaya, ushairi, vitabu vya watoto na tamthilia.
WASHINDI WA TUZO YA TAIFA YA UANDISHI BUNIFU WATAMBULIWA
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesisitiza dhamira yake ya kuendeleza Sekta ya elimu kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za waandishi bunifu na wachapishaji wa ndani.
WAZIRI MKUU NCHEMBA AWEKA JIWE LA MSINGI KAMPASI YA MZUMBE MKINGA
Leo tarehe 15 Februari 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili Mkoani Tanga, wilayani Mkinga ambako Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mkinga inajengwa ili kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi hiyo.
KAMPASI MPYA YA MZUMBE KUIMARISHA ELIMU NA UCHUMI WA TANGA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameielekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wadau wote kuhakikisha ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe katika eneo la Gombero wilayani Mkinga Mkoani Tanga unakamilika kwa wakati ili kuwezesha kuanza kwa mwaka mpya wa masomo Oktoba 2026.
KAMPASI MPYA ZAONGEZA UDAHILI NA WALIMU WA AMALI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, amesema kuwa ujenzi wa Kampasi 16 za vyuo vikuu nchini kupitia Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu kwa Uchumi (HEET) unalenga kupeleka fursa za elimu ya juu na hasa elimu ya ujuzi katika maeneo ya pembezoni.

