TUNAHITAJI WAWEKEZAJI ZAIDI KATIKA SEKTA YA ELIMU - PROF. MKENDA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yake huku ikiendelea kuvutia sekta binafsi na kusaidia uwekezaji wenye tija katika vyuo vikuu na kuongeza kuwa Serikali inahitaji wawekezaji zaidi ili kuimarisha maendeleo ya elimu nchini.

