BUNGE LAANZA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA ELIMU
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo leo Machi 13, 2026 imeanza ziara kukagua miradi ya elimu kwa lengo la kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma.

Kamati hiyo ikiwa mkoani Tanga, inatembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kampasi mpya ya Chuo Kikuu Mzumbe.
TANGA YAPOKEA BILIONI 27 KWA MIRADI YA ELIMU
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Sh. Bilioni 27 milioni 472 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu.
MKINGA NA MAONO YA GOMBERA KUWA MJI WA KIELIMU
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kupitia Mwenyekiti wake Mhe.Amani Juma Kasinga kwa kutenga eneo la kujenga mji wa wanazuoni katika eneo hilo.
UJENZI WA KAMPASI YA MZUMBE MKOANI TANGA WAFIKIA ASILIMIA 80
Ujenzi wa Kampasi ya Mzumbe katika eneo la Gomera Mkoani Tanga unaofadhiliwa na Benki ya dunia kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia umefikia asilimia 80.
KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MRADI WA KAMPASI YA MZUMBE TANGA
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu Utamaduni na Michezo imeridhishwa na uwepo wa mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe Gombero Wilayani Mkinga Mkoani humo.
VIJANA WANAPATA FURSA KUBWA KUPITIA UWEKEZAJI WA SERIKALI ELIMU YA JUU
SERIKALI YAONGEZA NGUVU KUBORESHA LISHE NA MAZINGIRA YA ELIMU
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir, ametoa wito kwa wadau wa elimu, wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bora na maji safi wakiwa shuleni ili kuboresha afya na kuongeza ufaulu kielimu.

