KAMPASI MPYA YA MZUMBE KUIMARISHA ELIMU NA MAGEUZI YA KIUCHUMI
Ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe katika eneo la Gombero wilayani Mkinga mkoani Tanga umeelezwa kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha fursa za upatikanaji wa elimu ya juu na kuchochea maendeleo ya Ukanda wa Kaskazini Mashariki.

