MWALIMU KOMBA AAHIDI USIMAMIZI BORA WA VIFAA VYA KIDIJITI

Mwalimu Komba wa Shule ya Sekondari Iyunga amesema kuwa Shule zilizopokea Vifaa vya Kidigitali vya kufundishia na kujifunzia watasimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuboresha elimu na ujuzi kwa vijana.



Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, kwa niaba ya shule zilizopokea vifaa Mwalimu Komba ameishukuru Serikali Kwa kuwapatia Vifaa hivyo vitakavyosaidia kwenye ufundishaji na ujifinzaji.

Swahili

TEKNOLOJIA ZA KIDIJITI KATIKA UJIFUNZAJI NI CHACHU YA MAGEUZI YA ELIMU - PROF. NOMBO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuboresha elimu nchini kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21.



Akizungumza Machi 30, 2026 Jijini Dodoma katika hafla ya ugawaji vifaa vya kidijitali, Prof. Nombo amesema kuwa lengo la pamoja kati ya Serikali na Wadau ni kuendeleza elimu na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika mfumo wa ufundishaji na ujifunzaji.

Swahili

NAIBU WAZIRI WANU AMEIR AGAWA VIFAA VYA KIDIJITI KWA SHULE ZA TANZANIA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir Machi 30, 2026 jijini Dodoma amewasili katika viwanja vya Ofisi za Wizara hiyo, kwa ajili ya kugawa Vifaa Vya Kijiditi vya Kufundishia na Kujifunzia katika Shule za Awali na Msingi na Shule za Sekondari nchini.



Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika sekta ya elimu na kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS