SERIKALI YASISTIZA MABORESHO YA ELIMU NA FURSA ZA KUJIFUNZA NDANI NA NJE YA NCHI
Tarehe 26 Machi, 2026 Mhe.Wanu Hafidh Ameir (Mb), Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini na kukutana na Watumishi wa Ubalozi pamoja na Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Kozi mbalimbali katika Vyuo Vikuu vilivyopo jijini Johannesburg na Pretoria.
WALIMU 150 WA AMALI ZA KIHANDISI KUONGEZA UMAHIRI INDIA
Tanzania imeandika ukurasa mpya katika historia ya elimu ya ufundi kwa kupeleka walimu 150 wa Amali za Kihandisi nchini India kwa mafunzo.

Hatua hii kubwa ya kimkakati siyo tu safari ya mafunzo, bali ni uwekezaji wa kitaifa katika mustakabali wa elimu na uchumi wa viwanda, ikilenga kuongeza umahiri wa walimu na kuandaa wataalamu watakaoshindana katika nyanja za teknolojia na uhandisi.
VIJANA 34 KUNUFAIKA NA UFADHILI WA MASOMO KATIKA CHUO KIKUU LIMERICK NCHINI IRELAND
Viijana 34 wanufaika wa Samia Scholarship Extended DS/SI + watanufaika na punguzo la ada ya masomo kwa asilimia 50 katika Chuo Kikuu cha Limerick cha Ireland, kufuatia makubaliano yaliyosainiwa Machi 26, 2026 jijini Dar es Salaam na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na chuo hicho.
TANZANIA, AFRIKA KUSINI KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIELIMU NA SAYANSI
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika ziara katika Chuo Kikuu cha Johannesburg nchini Afrika Kusini yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kielimu kati ya vyuo vya Tanzania na nchi hiyo.

