WANANCHI KATA YA MSINGISI WAFURAHIA UJENZI WA VETA GAIRO
Wananchi wa Kata ya Msingisi wilayani Gairo Mkoani Morogoro wameishukuru Serikali kwa kuwajengea VETA Gairo na kuiomba kuikamilisha ili vijana wa eneo hilo waweze kukitumia Chuo hicho kupata ujuzi.
WATANZANIA WATAKIWA KULINDA NA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MIRADI YA ELIMU INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI
KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UJENZI WA MAJENGO MAPYA KATIKA CHUO KIKUU CHA ARDHI
MLOGANZILA KUWA MJI WA TAALUMA NA TIBA
Serikali imedhamiria kuwa Kampasi ya Mloganzila ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) itakuwa mji wa kitaaluma na tiba, ikijumuisha vituo vya umahiri vitakavyotoa huduma za matibabu, elimu na utafiti ili kuimarisha sekta ya afya na elimu ya juu nchini.
KAMATI YA BUNGE YASIFU KASI YA UJENZI WA KAMPASI YA MLOGANZILA
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amekitaka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) kwa kushirikiana na Wizara kutangaza kuongeza kasi ya kuitangaza Kampasi ya Mlonganzila kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanyika.
UFUNGUZI WA KIWANDA MKURANGA KUONGEZA AJIRA NA UZALISHAJI
Ufunguzi wa kiwanda cha Federal Industry Limited kilichopo Mkuranga mkoani Pwani unatarajiwa kuongeza ajira kwa wananchi, kukuza uzalishaji na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi huo Machi 17, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wannnu Hafidh Ameir, amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa viwanda.

