Mhe. William Lukuvi aridhishwa na Ubora na Mazingira ya Jengo la Wizara ya Elimu Mtumba Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi Julai 23, 2025 Jijini Dodoma ameridhishwa na ubora na mazingira ya jengo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Amesema hayo alipotembelea Wizara akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya wizara na taasisi mbalimbali.

