MKENDA ATEMA CHECHE ZA SERA NA MITAALA YA ELIMU - TBC DAR ES SALAAM
MTAALA MPYA KUANZA MWAKANI 2024
MCHAKATO WA SERA YA ELIMU
Tunatambua na Kuthamini Waandishi Bunifu wa Ndani
Leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amepokea nakala ya kitabu kutoka kwa Mwandishi Elizabeth Mramba ambae pia ni Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Tunaendelea kuwapongeza Waandishi na kuhimiza Waandishi Bunifu kuwasilisha miswada ya kazi zao kushindania Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2023 mwisho wa kuwasilisha ni kesho tarehe 30 Novemba 2023.

PROF. MKENDA AHIMIZA UIMARISHAJI WA UBORA WA VYUO VIKUU AFRIKA
Mhe. Kipanga Jijini Nairobi, Akishiriki Mkutano wa Kenya Innovation Week 2023
Mhe. Omari Kipanga Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Jijini Nairobi, nchini Kenya akishiriki mkutano wa Kenya Innovation Week 2023 (KIW2023) - Commonwealth Edition.
Mkuatano unalenga kutoa fursa kwa nchi wanachama kubainisha hatua zinazochukua katika kukuza ubunifu. Pia mkutano utaweka mpango mkakati wa pamoja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola katika kuendeleza ubunifu.

Waziri Mkenda Azitaka Taasisi Elimu ya Juu Kushirikiana Kuimarisha Ubora wa Elimu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezitaka Taasisi za Vyuo Vikuu Barani Afrika kuendelea kushirikiana katika kuimarisha ubora wa Vyuo Vikuu.
Prof. Mkenda ametoa rai hiyo Novemba 28, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Mtandao wa Wadhibiti Ubora Barani Afrika (AfriQAN) unaoshughulikia masuala ya ubora katika elimu ya Juu, udhibiti na Usimamizi.
Tanzania na China Kuimarisha Ushirikiano Elimu ya Juu na Kati
Na WyEST
DSM
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo tarehe 27 Novemba, 2023 ameongoza Kikao kati ya Vyuo vikuu vya Ardhi, Dodoma, Mzumbe, Dar es Salaam, Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na ujumbe kutoka Chuo cha Jiingxi cha taaluma za kigeni nchini China.

