Gurnah awasili tayari kwa Tuzo za Uandishi Bunifu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Aprili 12, 2024 amempokea Mshindi wa Tuzo ya Nobel katika Fasihi Mwaka 2021 Prof. Abdurazack Gurnah ambaye anatarajiwa Mgeni Rasmi katika halfa ya utoaji Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2024



Prof. Gurnah amesema amefurahi kuwa sehemu ya tukio hilo kubwa muhimu katika uhamasishaji wa uandishi na usomaji wa vitabu nchini.

Swahili

Rais Samia mgeni rasmi kilele cha Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Tanga

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhitimisha Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.



Mkenda amesema hayo Machi 09, 2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema Maadhimisho hayo yatafanyika Mkoani Tanga kuanzia tarehe 25 hadi 31 Mei 2024 katika Viwanja vya Michezo vya Shule ya Sekondari Popatlal.

Swahili

Dkt. Biteko Mgeni Rasmi Mdahalo wa Kumbukizi Miaka 40 ya Hayati Sokoine

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo tarehe 8 Aprili, 2024 anashiriki katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya Miaka 40 ya Hayati Edward Sokoine unaofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mkoani Morogoro.



Mada kuu katika mdahalo huo ni "Urithi wa Taifa na Uongozi wake, Bidii, Uadilifu na Uaminifu."

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS