Wanafunzi katika Shule Zilikumbwa na Mafuriko Wataendelea na Masomo - Waziri Mkenda
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imejipanga na itahakikisha wanafunzi ambao shule zao zimefungwa kutokana na mafuriko Nchini kote wanaendelea na masomo.






