Prof. Carolyne Nombo Amekutana na Balozi wa Tanzania The Hague Nchini Uholanzi

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo April 28, 2024 amekutana na Balozi wa Tanzania The Hague Nchini Uholanzi Mhe. Caroline Kitana Chipeta kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu.



Prof. Nombo amemweleza Balozi huyo kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa mageuzi katika Elimu yanayolenga kuzalisha Wahitimu mahiri watakaoweza kushindana katika soko la ajira Kitaifa na Kimataifa.

Swahili

Tutaendelea Kushirikiana nanyi kwa Karibu Ikiwemu kuwa na Mifumo ya Kuwezesha Utekelezaji Kupitia Public Private Partnership.

Napenda kushukuru Wawekezaji Binafsi katika sekta ya elimu nasisitiza kuwa tutaendelea kushirikiana nanyi kwa karibu ikiwemu kuwa na mifumo ya kuwezesha utekelezaji kupitia Public Private Petnership.



Aidha, tunataka Mafunzo ya Amali yawezeshe Ujuzi kwa Wahitimu, hivyo tutahakikisha yanatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa, hivyo tunahimiza Shule kuwekeza katika miundo mbinu na vifaa stahiki vya mafunzo ya amali inayotoa.

Swahili

Prof. Adolf Mkenda ameungana na familia na viongozi mbalimbali katika mazishi ya Mtangazaji wa Clouds FM marehemu Gadner G Habash

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameungana na familia na viongozi mbalimbali katika mazishi ya Mtangazaji wa Clouds FM marehemu Gadner G Habash Wilayani Rombo, Kilimanjaro



Tunatoa pole kwa Clouds FM ambao tunashirikiana katika kampeni mbalimbali za uhamasishaji na elimu kwa umma juu ya masuala ya elimu, marehemu akiwa mmoja wa watangazaji walioshiriki katika kuendesha kampeni hizo

Swahili

Prof. Nombo Asisitiza Uwajibikaji katika Kuhudumia Wateja

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi na kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwahudumia ipasavyo wateja wao kwa kutumia mifumo iliyopo.

Prof. Nombo ametoa rai hiyo Aprili 24, 2024 Mkoani Morogoro, wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Mkutano wa 33 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara huku akisisitiza Watumishi wote kutoa huduma bora kwa wateja.

Swahili

Kipanga Ahudhuria Ufunguzi wa Kongamano la Sita la Paset na Rsif Nairobi Kenya

Na
WyEST
Nairobi , Kenya
Aprili, 2024

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Juma Kipanga akifuatilia ufunguzi wa Kongamano la sita la Partneship for Skills in Apllied Sciences and Engineering Technology (PASET) na (RSIF) Regional Scholarship and Innovation Fund linalofanyika Nairobi Kenya.



PASET ni ushirika unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ukiwa na wanachama 25 kutoka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Swahili

UNICEF watoa Msaada wa Vifaa vya Kielimu kwa Shule Zilizoathiriwa na Mafuriko

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughukia Watoto (UNICEF) April 24, 2024 limekabidhi vifaa vya kielimu kwa ajili ya Wanafunzi na Walimu wa Shule zilizoathiriwa na mafuriko yanayotokana na mvua zinazoendelea katika Wilaya ya Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya Kibiti Kanali Joseph Kolombo.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS