WANANCHI NJOMBE WAPONGEZWA KUCHANGIA MAENDELEO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Septemba 20, 2024 ameongea na wananchi wa Kata ya Makowo mkoani Njombe baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari Makowo.
Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kusimamia zoezi la ubainishaji na kuhakikisha Watoto wenye mahitaji maalum wanaandikishwa shule
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu) Atupele Mwambene amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kusimamia zoezi la ubainishaji na kuhakikisha Watoto wenye mahitaji maalum wanaandikishwa shule na kupatiwa afua stahiki kulingana na mahitaji yao.
SERA YA ELIMU IMEZINGATIA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM DKT. MAHERA
Serikali imeanza kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, pamoja na Mitaala iliyoboreshwa kwa kuzingatia ujumuishwaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ngazi zote za elimu.
KASI YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA ,SHULE YA SEKONDARI YA KWANZA MAKOWO YAJENGWA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya kwanza katika kata ya Makowo, shule ya Sekondari Makowo iliyojengwa kupitia Mradi wa kuendeleza Elimu ya Sekondari (SEQUIP)
NJOMBE YAJIVUNIA KUPATA KAMPASI YA CHUO KIKUU
Njombe yajivunia kupata Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinachojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambayo itakuwa Taasisi ya Kwanza ya Elimu ya Juu katika mkoa huo.
Sera ya Elimu imezingatia Stahiki kwa wenye Mahitaji Maalum
Mkurugenzi wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Magreth Matonya amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 imezingatia stahiki mbalimbali kwa wenye mahitaji Maalum kuhakikisha wanapata elimu bora kuchochea maendeleo yao.
Dkt. Wilson Charles Mahera Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Elimu Jumuishi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Charles Mahera Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Elimu Jumuishi akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Maadhimisho haya yanasherekewa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Patandi Maalam jijini Arusha
Wanafunzi katika Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 30 ya Elimu Jumuishi
Wanafunzi katika Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 30 ya Elimu Jumuishi katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Patandi Maalam jijini Arusha.

Kauli mbiu: Elimu Jumuishi inayozingatia maadili, ujuzi, ubunifu na teknolojia kuleta usawa na maendeleo ya wote
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewasili Mkoani Njombe tayari kuanza ziara ya kikazi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewasili Mkoani Njombe tayari kuanza ziara ya kikazi katika Wilaya zote mkoani humo.

Lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.na kuzugumza na Wananachi


