WATAKAOJIUNGA ELIMU YA AMALI KUSOMA MASOMO MATANO YA LAZIMA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Caroylne Nombo amesema kuwa Wanafunzi wanaosoma Mkondo wa Amali watalazimika kusoma masoma matano ya lazima pamoja na moja la fani.



Akizungumza Septemba 26, 2024 Mkoani Ruvuma wakati wa uwasilishaji wa mada ya Mageuzi katika Sekta ya elimu kwa wajumbe wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa kwa Viongozi wa Kisiasa Wanawake Tanzania, amesema kuwa fani kuu katika mkondo huo ni 15.

Swahili

PROF. MKENDA NA PROF. NOMBO WAKABIDHI NAKALA YA VITABU VYA SERA UWT

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Septemba 26, 2024 imekabidhi nakala ya Vitabu vya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kwa Viongozi wa Kisiasa Wanawake Tanzania.



Makabidhiano hayo yamefanywa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo Mkoani Ruvuma wakati wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa kwa Viongozi hao yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).

Swahili

Mhe. Omari Kipanga ameanza ziara ya kikazi Mkoa wa Mara

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga ameanza ziara ya kikazi Mkoa wa Mara kukagua miradi ya ujenzi inayotekekezwa na Wizara katika Mkoa huo



Mhe. Kipanga Septemba 25, 2024 amefika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Kukutana Mkuu wa wilaya hiyo Mh. Dkt Vicent Anney kabla ya kuelekea Kukagua Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya hiyo

Swahili

KIPANGA AWATAKA WAKANDARASI UJENZI VETA BUNDA KUZINGATIA UBORA

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe Omari Kipanga amewataka Wahandisi wa ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Bunda kuzingatia ubora wa kazi na ramani za majengo.



Kipanga amesema Chuo hicho cha Bunda ni miongoni mwa Vyuo 64 vinavyojengwa kwa kupitia agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kila wilaya ya Tanzania bara inajengewa Chuo cha Ufundi na mafunzo ya ufundii stadi cha Wilaya

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS