SHULE YA MSINGI YA CHIEF ZULU YA MKONDO WA KIINGEREZA YAZINDULIWA SONGEA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Shule ya Msingi Chief Zulu inayofundisha kwa lugha ya Kiingereza

Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba 24, 2024 Mkoani Ruvuma ambapo Mhe. Rais amewataka Mawaziri wanaoshughulikia Elimu kuhakikisha walimu wenye uwezo wa kufundisha vizuri kwa kutumia lugha ya Kiingereza wanapatikana hata kutoka nje ya nchi.

Swahili

Wizara inashirikiana kikamilifu na Shirika linaloshughulika na Kampeni ya Elimu kwa Mtoto wa Kike CAMFED

Naibu Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera amesema Wizara inashirikiana kikamilifu na Shirika linaloshughulika na Kampeni ya Elimu kwa Mtoto wa Kike (CAMFED) katika kuhakikisha Wanafunzi waliokatisha masomo wanapata fursa ya elimu na ujifunzaji kuwezesha kufikia malengo yao.

Swahili

WyEST inaendelea kutoa mafunzo kwa watekelezaji na wasimamizi wa Miradi inayoratibiwa na kusimamiwa chini yake.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kutoa mafunzo kwa watekelezaji na wasimamizi wa Miradi inayoratibiwa na kusimamiwa chini yake.



Septemba 23, 2024 ilianza kutoa Mafunzo kwa Wasimamizi na Watekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) juu ya namna ya kuzingatia masuala ya Jamii, Jinsia, Mazingira na Ujumuishi wakati wa utekelezaji. Mafunzo hayo ni ya siku tano yanafanyika Bagamoyo.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS