SHULE ZINAONGOZWA KWA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI

Na WyEST
 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.  Adolf Mkenda amesema wizara imetuma wathibiti ubora wa shule katika shule ya Msingi Izinga iliyo Nkasi kufuatilia taarifa zinazosambaa kwamba walimu wamefukuza wanafunzi ambao wazazi wao ni wanachama cha CHADEMA.

Waziri huyo amesisitiza kuwa vyama vipo kwa mujibu wa sheri na kwamba shule zinaongozwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na kwamba hakuna muongozo unaosema mwanafunzi atengwe kwa mlengo wa kisiasa

Swahili

SERIKALI INAYOONGOZWA NA MHE SAMIA IMEJENGA NA KUKARABATI MIUNDOMBINU INAYOZINGATIA MAHITAJI MAALUM YA WANAFUNZI KUANZIA ELIMU YA AWALI MPAKA VYUO VIKUU

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Hamis Nderiananga amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga na kukarabati miundombinu inayozingatia mahitaji maalum ya wanafunzi kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu



Ameyasema hayo leo Disemba 5 2024 Mkoani Morogoro kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Mawaden 147 kutoka kwenye Taasisi za Elimu ya juu zinazopokea Wanafunzi wenye mahitaji Maalum

Swahili

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAKABIDHIWA VYUO 10 VYA UFUNDI STADI NA MAREKEBISHO KWA WENYE ULEMAVU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amepokea Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Makabidhiano hayo yamefanyika Disemba 04, 2024 Jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho cha Yombo kati ya Naibu Katibu Mkuu huyo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS