Prof. Daniel Mushi amekagua ujenzi wa miundombinu katika Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi Januari 11, 2025 amekagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE) inayotekelezwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Majengo yaliyokaguliwa ni pamoja na Jengo la Sayansi, Jengo la Multimedia na Elimu Maalum, jengo la Maabara ya Fizikia, maktaba na hosteli ambapo ujenzi umefikia asilimia 12.



