Prof Carolyne Nombo amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Kukuza Usafirishaji wa Huduma Nje (Service Export Promotion Council)

Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Kukuza Usafirishaji wa Huduma Nje (Service Export Promotion Council) Dkt. Abhay Sinha.


Katika mazungumzo hayo, wamekubaliana kuingia mshirikiano yatakayowezesha maendeleo ya ujuzi

Swahili

Tanzania na India zakubaliana kushirikiana katika kuandaa nguvu kazi yenye Ujuzi unaohitajika katika nchi zote mbili

Tanzania na India zakubaliana kushirikiana katika kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi unaohitajika katika nchi zote mbili kupitia elimu ya Ufundi na Ufundi stadi.

Makubaliano hayo yamefanyika Januari 14, 2025 nchini India kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujuzi na Ujasiriamali nchini India Atul Kumar Tiwari

Swahili

Prof. Carolyne Nombo ameongoza ujumbe wa Wizara katika ziara ya Ulinganishaji (benchmaking) nchini India

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameongoza ujumbe wa Wizara katika ziara ya Ulinganishaji (benchmaking) nchini India.



Katika ziara hiyo, Prof. Nombo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vyama vya Vyuo Vikuu nchini India ambapo wamekuabaliana kuingia mashirikiano kati ya Vyuo vikuu vya India na Vyuo vikuu vya Tanzania katika maeneo mbalimbali

Swahili

WANAFUNZI WA KIKE 12,000 WALIOKATIZA MASOMO KURUDI SHULENI

Serikali imedhamiria kuwarudisha Wasichana 12,000 walikatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali katika mfumo wa elimu kwa njia mbadala.



Hayo yameelezwa Januari 13, 2025 mkoani Morogoro na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizindua Warsha ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa SEQUIP AEP, ambapo ameipongeza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kuendelea kuboresha elimu nchini.

Swahili

Prof. Carolyne Nombo amekutana na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Anisa Kapufi Mbega

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Januri 13, 2025 amekutana na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Anisa Kapufi Mbega kwa ajili ya kumshirikisha malengo ya ziara ya kiongozi huyo nchini humo pamoja na kuelekezana masuala kadhaa yanayohusu sekta ya elimu.



Prof. Nombo amemueleza Balozi huyo juu ya Mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini Tanzania.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS