Dkt. Rwezimula ahimiza matumizi ya TEHAMA kwenye mafunzo ya Ufundi Stadi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amehimiza matumizi ya TEHAMA kwenye mafunzo ya Llfundi Standi ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia na mahitaji ya soko kwa wahitimu wa mafunzo hayo.

Ametoa rai hiyo wakati wa Ziara yake mkoani Kilimanjaro alipotembelea Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Moshi na kujionea wanafunzi Wakiendelea na mafunzo kwa vitendo.

Swahili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mhandisi wa Mtaani (Street Engineer) Adam Zacharia Kinyekile kutoka Tunduma Mkoani Songwe aliebuni na kutengeneza mashine hiyo ya kuvuta maji, kupukuchua mahindi, kusaga nafaka pamoja na kubeba Mizigo na ubunifu wake kuendelezwa na COSTECH katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Swahili

Mkenda Asisitiza Uwekezaji katika Sayansi na Teknolojia

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekitaka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kuwekeza kwenye Sayansi na Teknolojia ili kuchangia katika kuinuia uchumi..

Prof. Mkenda ametoa rai hiyo Agosti 7, 2023 wakati akizungumza na Viongozi na Wafanyakazi wa Chuo hicho baada ya kutembelea na kujionea Maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na MUST.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS