Dkt. Rwezimula Awataka Wathibitu Ubora Kufanya kazi kwa Bidii

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula leo Agosti 28, 2023 amekutana na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda ya Dar es Salaam.

Akizungumza na Wathibiti Ubora hao Dkt. Rwezimula amewataka kufanya kazi kwa bidii na weledi katika kutimiza majukumu yao.

Naibu Katibu Mkuu huyo yupo Mkoani Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa Veta mpya zinazojengwa mkoani humo

 

Swahili

Mkenda ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Uru - Kilimanjaro

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Uru kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

Pongezi hizo amezitoa Agosti 26, 2024 Mkoani Kilimanjaro akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki

Prof. Mkenda amesema kuwa kufanya vizuri kwa shule hiyo ni kutokana na jitihada za walimu na wanafunzi pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule na wazazi.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS