WILAYA YA MWANGA KUPATA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda June 5, 2025 amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, ambapo ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kilaweni Usangi.

Katika ziara hiyo wananchi wa Mwanga wakiwakilishwa na Mbunge wao Mhe. Joseph Thadayo wamemuomba Prof. Adolf Mkenda kwa mamlaka aliyonayo aifanye shule hiyo iwe moja ya shule ya amali.

