Waziri mkenda atambulisha timu ya kupitia utaratibu utoaji mikopo elimu ya juu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Septemba 5, 2022 ameitambulisha rasmi  kwa Bodi na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) timu itakayofanya mapitio ya utaratibu wa utoaji mikopo kwa miaka mitano iliyopita ili kuona namna ya  kuboresho utaratibu huo.

Swahili

Prof. Nombo awataka wadau wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kushiriki kutoa maoni kwa maslahi ya taifa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema mapitio na mabadiliko ya Sera ya Sayansi Teknolojia ya mwaka 1996 yanafanyika ili kuakisi mahitaji na kasi ya mabadiliko ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini. 


Prof. Nombo amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Kikao kazi cha kujadili na kupokea maoni hya wadau juu ya Rasimu ya Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi cha Uratibu wa masuala ya Ubunifu nchini.

Swahili

TCU watakiwa kusimamia ubora elimu ya juu

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh.Omari Kipanga ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuongeza jitihada  katika uthibiti wa Ubora wa vyuo vikuu ili kuwaandaa wahitimu kushindana katika soko la ajira.

Akizungumza leo Agosti 17 mjini Morogoro wakati akifungua  Mafunzo ya kuandaa Mitaala inayoendana na Soko la Ajira, Mh. Kipanga alisema kwamba hatua hiyo itawezesha vyuo kufuata taratibu zilizowekwa na kutoa elimu iliyokusudiwa.

Swahili

Bilioni 100 Kuimarisha elimu ya Ufundi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejizatiti katika kutoa elimu ujuzi na hivyo itaendelea kuwekeza katika elimu ya ufundi ikiwemo ujenzi wa Vyuo vya VETA  katika kila wilaya na Mikoa.

Amesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mbarali kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia chini ya Mradi wa Kukuza Ujuzi (ESPJ).

Swahili

Shule zenye changamoto ya miundombinu kunufaika na mfuko wa elimu wa taifa

Shule zenye uhaba mkubwa wa miundombinu unaotokana na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi na zilizosajiliwa zinatarajia kunufaika na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Hayo yameleezwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari - MAELEZO kuhusu utekelezaji na mwelekeo wa Bajeti ya TEA kwa mwaka 2022/23.

Swahili

Tangazo la nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada ya ualimu elimu ya sekondari kwa mwaka wa masomo 2022/2023

1. UTANGULIZI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha SITA wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

2. SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS