Waziri Mkenda afanya mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Juu kutoka Afrika Kusini

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kutoka Afrika Kusini Dkt. Bonginkosi Nzimande juu ya ushirikiano katika Nyanja za elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia na Utafiti.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Nzimande amemuomba Waziri Mkenda kukamilishwa kwa mapendekezo ya mkataba wa makubaliano kati ya Tanzania na Afrika Kusini kuhusu ushirikiano wa elimu ya Juu na Mafunzo ya Ufundi stadi.

Swahili

Viongozi wa WyEST wamekutana na wajumbe wa Benki ya Dunia

Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wamekutana kwa mara ingine na kufanya majadiliano na ujumbe wa Benki ya Dunia juu ya ushirikiano katika utekelezaji wa mageuzi makubwa ya elimu nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imekamilisha Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na maboresho ya mitaala ya elimu.

Swahili

Pages

Subscribe to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia RSS