MRADI WA UWEZESHAJI KUPITIA UJUZI (ESP) UTAWAINUA VIJANA KIUCHUMI
Mkenda azindua Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Vijana Vyuoni
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf amesema serikali inazingatia suala la Usalama na Ulinzi wa watoto katika Taasisi za Elimu na Vyuo, kuhakikisha hakuna unyanyasaji wa kijinsia.
Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Julai 22, 2023 wakati akizindua Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Vijana katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs), Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Mkenda asimikwa kuwa miongoni wa wazee wakimila ya kimaasai- Mto wa Mbu FDC
Katika halfa ya Uzinduzi wa Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Vijana katika Taasisi za Vyuo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda atawazwa kuwa mmoja wa Viongozi wa Heshima katika Wazee wa Kimasai _Olaigwanani_
Diwani wa Kata ya Esilalei Mhe. Lemia Mollel amemvalisha vazi maalum Waziri huyo na kumkabidhi rungu kuashiria Mamlaka hayo ya kimila.

PROF. CAROLYNE NOMBO
Dkt. Hussein Mohamed Omar,
MHe. OMARY KIPANGA
MHE. PROF ADOLF MKENDA
NBC YATOA UFADHILI KWA WANAFUNZI 1000 VETA
NBC Yatoa Ufadhili kwa Wanafunzi 1,000 VETA
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini mkataba wa Makubaliano ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa ufadhili huo unakwenda kutimiza azma ya Serikali ya kutoa Elimu na Mafunzo yatakayo wawezesha vijana wa kitanzania kupata ujuzi wa kujiajiri ama kuajiriwa.

