1.    UTANGULIZI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi. Mafunzo yatakayotolewa ni Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 02) pamoja na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali Msingi na Elimu Maalumu (miaka 02) ni wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III).

Waombaji wa nafasi za mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Mafunzo haya yatatolewa katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali. Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

2.    SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

a)    Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) ni:

  1.  Wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass”mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali.
  2.  Walimu waliohitimu Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali au Msingi. Aidha waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa, watapangwa kwenye mikondo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu ya Ualimu. 

b)    Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni: Basic Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science

  1. AINA YA MAFUNZO NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO

Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya Mafunzo ya Ualimu (kozi) na vyuo vinavyotoa mafunzo husika.

  1. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI NA MSINGI (MIAKA 02)

Na.

AINA YA MAFUNZO (KOZI)

VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO

Vya Serikali

Visivyo vya Serikali

1

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya Jamii (kwa kutumia lugha ya kiswahili)

Mhonda, Murutunguru, Ngorongoro na Vikindu.

Al harmain, Darmiki, Nyamwezi, Montessori Kawekamo, St. Aggrey Chanji, Mong’are, Lake,Bishorp Daniel, King Rumanyika, Kilimanjaro modern,  Kirinjiko na King’ori

2

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya Jamii (kwa kutumia lugha ya Kiingereza)

Mpuguso, Shinyanga.

 

 

UCA na Lake

3

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya jamii na lugha ya kiswahili (kwa kutumia lugha ya kiswahili).

 

Bunda, Tandala,

St. Aggrey, Sila, St. Marys, Coast, Green bird, Nazareth, Teki, St. Maurus, Arafah, Kisongo, Mwl. Franz, St. Francis Nkindo, Sahara, Mbeya Moravian, Rukwa, Ebonite, Arusha, DC Brilliant, Mtumba, Musoma Utalii, Lua na Partage Montessori.

4

Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu (kwa kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza)

Patandi.

 

 

5

Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu (kwa kutumia lugha ya kiswahili)

Kabanga, Mpwapwa.

 

 

6

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi na Hisabati (kwa kutumia lugha ya kiingereza)

Ndala, Mandaka, Mamire.

 

UCA

 

 

8

 

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi na Hisabati (kwa kutumia lugha ya kiswahili) 

 

Kitangali, Bustani, Ngorongoro na Sumbawanga

St. Aggrey, Sila, St. Marys, Coast, Green bird, Tofilo Kisanji, St. Maurus, Arafah, Kisongo, Mwl. Franz, St. Francis Nkindo, Nyamwezi, Sahara, Mbeya Moravian, Rukwa, Ebonite, Arusha, DC Brilliant, Mtumba, Montessori Kawekamo, Musoma Utalii,  Al harmain, St. Aggrey Chanji, Lake, Bishorp Daniel, King’ori, Kirinjiko, King Rumanyika, Kilimanjaro modern na Partage Montessori.

9

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali (kwa kutumia lugha ya kiingereza)

Dakawa, Nachingwea.

UCA

10

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali (kwa kutumia lugha ya kiswahili) 

Kinampanda, Katoke,

Singachini.

Darmiki, King Rumanyika  na Kilimanjaro modern

11

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa lugha (Kiingereza, Kifaransa na Kichina)

Marangu. 

Arafah, St. Aggrey Chanji, UCA, King’ori, Bishorp Daniel, King Rumanyika, Nyamwezi, Al harmain, Kilimanjaro modern na Montessori Kawekamo

12

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sanaa na Michezo (kwa kutumia lugha ya Kiingereza)

Butimba. 

 

13

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sanaa na Michezo (kwa kutumia lugha ya kiswahili) 

Ilonga na Tarime.

Lake, Montessori Kawekamo, King Rumanyika, Coast, Nyamwezi na Musoma Utalii

 

  1.  
  2.  
  3.  
  4.  
  5.  
  6.  
  7. STASHAHADA MAALUMU YA UALIMU ELIMU YA MSINGI KATIKA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI (MIAKA 03)

 

Na

AINA YA MCHEPUO

VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO

1.              

PME, CBE, CME na CSME

Tukuyu

 

2.              

PME, PCE, PBE, CBE, CME na CSME 

Morogoro, Kasulu, Songea, Korogwe na Tabora

 

3.              

PME, PCE, PBE, CME na CBE

Klerruu na Monduli

 

 

 

4.      UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NA KUPOKEA MAJIBU

Utaratibu wa kutuma maombi na kupokea majibu utakuwa kama ifuatavyo:

(i)      Wahitimu wa Kidato cha nne, Kidato cha sita na Walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi, wenye sifa zilizobainishwa katika tangazo hili  wanaruhusiwa kutuma maombi;

(ii)    Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://tcm.moe.go.tz/);

(iii)   Mwombaji  wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua kozi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;

(iv)   Mwombaji  wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;

(v)    Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kwenye mfumo kupitia “Account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia tarehe 20/07/2025) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa

(vi)    Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo visivyo vya Serikali  watatuma maombi yao  katika vyuo  husika. Aidha, majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo hayo  yatatolewa na  Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa; na,

(vii) Fomu  za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.

 

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10/07/2025.