MRADI WA KUJENGA UJUZI NA USHIRIKIANO AFRIKA MASHARIKI “EAST AFRICA SKILLS FOR TRANSFORMATION AND REGIONAL INTEGRATION PROJECT

(EASTRIP)

 

  1. UTANGULIZI:

Mradi wa kujenga ujuzi na ushirikiano Afrika Mashariki “EAST AFRICA SKILLS FOR TRANSFORMATION AND REGIONAL INTEGRATION PROJECT (EASTRIP) ni Mradi ambao unatakelezwa kupitia fedha za mkopo wa masharti nafuu wa Benki ya Dunia (Worl Bank). Mradi huo uliidhinishwa na bodi ya Benki ya Dunia mnamo Oktoba 2018 na umeanza kutekelezwa tangu Machi 2019 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2024. Mradi huu umeshirikisha Nchi Tatu yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kenya na Ethiopia. Kwa Nchi zote zote tatu kwa ujumla zinatekeleza mradi katika vituo vya umahiri kumi na sita (16) kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali hapo chini:

Sekta

Eneo la Kisekta

Chuo

Nchi

TRANSPORT/

INFRASTRUCTURE

 

Reli

Meles Zenawi Memorial TVET Polytechnic College

Ethiopia

Reli

Ethiopia Railway Academy

Ethiopia

Maji

Kenya Coast National Polytechnic

Kenya

Anga

National Institute of Transport

Tanzania

Barabara

Kombolcha TVET Polytechnic College

Ethiopia

Ujenzi

Meru National Polytechnic

Kenya

“Highway infrastructure”

Kenya Institute of Highway and Building Technology

Kenya

POWER/ENERGY

 

Power/energy

General Wingate Polytechnic College

Ethiopia

Geothermal

KenGen Geothermal Training Center

Kenya

Hydro

Arusha Technical College

Tanzania

MANUFACTURING

 

Tool making/leather

TVET Institute

Ethiopia

Textile/garment

Hawassa TVET Polytechnic College

Ethiopia

Textile

Kisumu National Polytechnic

Kenya

Leather

DIT Mwanza Campus

Tanzania

Agro-processing

Holeta TVET Polytechnic College

Ethiopia

ICT

ICT

DIT Dar es Salaam Campus

Tanzania

 

Nchini Tanzania, mradi huu unatekelezwa kwa kuendeleza/kujenga vituo vinne (4) vya ubora kama ifuatavyo:

  •  Taasisi ya Teknolojia kampasi ya Dar es Salaam -  Kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya TEHAMA (RAFIC) iliyotengewa Dola za Kimarekani Milioni 16.25)
  • Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya Taaluma za Anga na Operesheni za Usafirishaji (CoEATO) iliyotengewa Dola za Kimarekani Milioni 21.25
  • Chuo cha Ufundi Arusha - Kituo cha Mafunzo na Utafiti wa Nishati Jadidifu (KIKULETWA) kilichotengewa Dola za Kimarekani Milioni 16.25
  • Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kampasi ya mwanza - Kituo cha umahiri cha Uchakataji Ngozi (CELPAT) iliyotengewa Dola za Kimarekani Milioni 16.25.
  • Bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Wizara ni Dola za Kimarekani Milioni 5 kwa ajili ya kukamilisha shughuli zake .

Vituo hivi vilipokea fedha miezi 9 baada ya tarehe ya utekelezaji (Februari, 2020) na Wizara ilipokea fedha baada ya miezi 18 (Novemba, 2020)

 

2.         LENGO LA MAENDELEO YA MRADI

 Lengo Kuu:

Kuongeza UPATIKANAJI na KUBORESHA UBORA wa programu za TVET katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi vya Kikanda (TVET) kwa kuanzisha Vituo vya Umahiri  vitakavyosaidia kuongeza ushirikiano wa Kikanda.

Lengo la mradi wa EASTRIP litafikiwa kwa usimamizi uliodhibitiwa na umeundwa katika ngazi tatu zifuatazo:

  1. Taasisi za TVET za Kikanda (RFTIs- Regional Flagship TVET Institutions) zitahusika na utekelezaji wa mradi katika ngazi ya taasisi.

Taasisi hizi zitaanzisha Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi (PIU) kwa ajili ya kupanga mikakati na utekelezaji wa mipango iliyoidhinishwa, kwa kuzingatia kazi za msingi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa mradi, kiufundi, uhusiano wa sekta, uaminifu, na ulinzi ikiwa ni pamoja na lengo la jinsia, M & E, na mahitaji mengine kama kutathminiwa na kupendekezwa na Benki ya Dunia na kukubaliana na wenzao.

Zaidi ya hayo, Bodi/Kamati ya Ushauri wa Viwanda itaanzishwa ama katika ngazi ya taasisi au katika ngazi mahususi ya kituo ili kutoa mwongozo kuhusu ushirikiano wa sekta na kubuni programu mahususi za ushirikiano na sekta hiyo.

  1. Vitengo vya Kitaifa vya Uratibu wa Miradi (NPCU-National Project Coordination Unit) vimeanzishwa katika Wizara ya Elimu nchini Ethiopia na Kenya na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania yenye majukumu muhimu ya mradi ikiwa ni pamoja na uratibu wa Miradi, Ununuzi, Usimamizi wa Fedha, na ufuatiliaji na tathmini. Aidha Wizara zinaandaa Miongozo mbalimbali, Sera, kuwezesha mikutano, maonesho, mashindano na semina,  kuwezesha baadhi ya watumishi katika programu za muda mrefu na mfupi.
  2. RFU –Regional flagship unit (the Inter-University Council for East Africa, IUCEA, in Uganda)), inazisaidia taasisi za TVET na NPCU katika utekelezaji wa mradi. Zaidi ya hayo, RFU inatekeleza mipango ya Kikanda ya mradi. Inatoa ushauri na uratibu wa shughuli za mradi kiujumla.