
Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Ualimu (TESP)
Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Ualimu (TESP) ni mpango wa miaka nane (2017–2025) unaotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ushirikiano na Serikali ya Kanada kupitia Global Affairs Canada (GAC).
Lengo kuu la Mradi ni kuongeza ubora, usawa, ujumuishi na uendelevu wa elimu ya Ualimu wa shule za msingi na sekondari nchini Tanzania. Mradi huu unatekelezwa kwa msaada wa washauri elekezi kutoka Alinea International kupitia “TA-TESP”.
Mradi huu umegharimu, Dola za Kanada milioni 53 na ufadhaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Kanada.
Malengo Makuu ya Mradi
- Kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika vyuo 35 vya ualimu vya Serikali kuwa rafiki na Jumuishi.
- Kuboresha mitaala ya mafunzo ya ualimu ili iwe jumuishi, shirikishi, na iendane na mahitaji ya sasa ya elimu na mabadiliko ya tabianchi na teknolojia.
- Kuwezesha walimu tarajali na waliopo kazini kupata mafunzo endelevu, yanayozingatia TEHAMA, jinsia, na ujumuishaji
- Kukuza matumizi endelevu na salama ya TEHAMA na kwa kuzingatia usimamizi wa taka za kielektroniki (e-waste), matumizi ya nishati, na mbinu za kidijitali zisizohitaji uchapishaji.
- Kuweka msingi wa utoaji elimu ya ualimu inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo ya kijani (green or eco design)
Walengwa wa Mradi
- Wakufunzi katika vyuo 35 vya Ualimu vya Serikali
- Walimu tarajali katika vyuo 35 vya Ualimu vya Serikali
- Taasisi za kielimu ambazo ni Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Chuo cha Maendeleo ya Elimu (ADEM) na Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA).
- Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutokana na walimu waliopata mafunzo bora
- Wadau wa sekta binafsi na asasi za kiraia katika Elimu
Maeneo ya Utekelezaji wa TESP
- Vyuo vya Ualimu vya Serikali (35)
- Chuo cha Ualimu Kabanga kimejengwa upya kwa gharama ya TZS bilioni 12. Ni Chuo cha mfano wa usanifu wa kijani (climate-resilient & green design) unaozingatia ufanisi wa nishati, usalama wa kiafya na mazingira rafiki kwa walimu na wanafunzi
- Ujenzi wa maktaba, maabara, mabweni, na miundombinu rafiki kwa mazingira
- Kuwezesha matumizi ya TEHAMA rafiki kwa mazingira
- Kutoa vifaa vya kufundishia na kufundishia kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na ujumuishi
- Kuimarisha uwezo wa wakufunzi kwa mbinu shirikishi na matumizi ya TEHAMA
- Uimarishaji Taasisi za Kitaifa za Elimu
- TIE - mapitio ya mitaala ya ualimu yenye mwelekeo wa ujumuishaji, jinsia na mabadiliko ya tabianchi
- ADEM - mafunzo ya viongozi wa vyuo - usimamizi jumuishi na endelevu wa elimu
- NECTA - kuboresha mfumo wa ukaguzi na usahihishaji mitihani kwa njia ya kielektroniki (E-marking).
- Uboreshaji elimu ya Msingi na Sekondari
- Mafunzo ya kazini kwa walimu waliopo katika hisabati, TEHAMA na elimu jumuishi
- Mazingira salama na rafiki ya elimu kwa watoto wote
- Kuongeza Ufaulu Halmashauri zenye Ufaulu Duni
Mafunzo mahsusi yametolewa kwa walimu katika Halmashauri 20 ili kuongeza ufaulu, hasa katika Hisabati na Elimu Jumuishi
Matokeo Tarajiwa ya Mradi
i) Matokeo ya Muda Mfupi (Immediate Outcomes)
- Wakufunzi wamepata ujuzi mpya wa kufundisha kwa njia jumuishi na kidijitali
- Mitaala ya Ualimu imeboreshwa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi, ujumuishaji na TEHAMA
- Miundombinu ya Vyuo imeimarishwa kwa usanifu wa kijani na ufanisi wa nishati
- Taasisi za elimu zimewezeshwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na uendelevu
ii) Matokeo ya Kati (Intermediate Outcomes)
- Kuongea ubora wa mafunzo ya ualimu kupitia mitaala jumuishi na rafiki kwa mazingira
- Kuimarika uendeshaji wa vyuo umeimarika kwa mifumo madhubuti ya ufuatiliaji
- Walimu waliopo kazini wameongezewa wa uwezo na ujuzi kupitia mafunzo ya elimu jumuishi na TEHAMA
iii) Matokeo ya Mwisho (Ultimate Outcome)
Kuimarika kwa uwezo wa walimu kufundisha kwa ufanisi katika mazingira jumuishi na rafiki kwa tabianchi, kwa kutumia mbinu shirikishi na TEHAMA.
Mafanikio Makuu ya Mradi
- Ujenzi wa Chuo cha Kabanga – mfano wa usanifu wa kijani na usalama wa tabianchi
- Maktaba, maabara na madarasa 7 yameboreshwa
- Vitabu na vifaa vya TEHAMA zaidi ya 196,000 vimesambazwa
- Wakufunzi 5,900 wamefunzwa mbinu shirikishi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na ujumuishi na TEHAM
- Mfumo wa E-marking umeanzishwa NECTA
- Mtaala wa ualimu umehuishwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania
Masomo Tuliyojifunza (lessons learnt) Kupitia utekelezaji Mradi wa TESP
- TEHAMA imeongeza ubora wa elimu lakini inahitaji usimamizi wa e-waste na matumizi ya nishati
- Mafunzo kwa vitendo (BTP) yametoa uzoefu halisi kwa walimu tarajali
- Mafunzo ya lugha ya alama na usambazaji wa taulo za kike yameimarisha ujumuishaji
- Upatikanaji wa vifaa na miundombinu rafiki kwa mazingira umeongeza ubora wa kujifunza
- Maktaba za kidijitali zimeongeza upatikanaji wa maarifa bila uchapishaji
- Uwezeshaji wa wakufunzi umeimarisha mbinu za kisasa za ufundishaji
- Ubunifu wa wanafunzi umeongezeka kupitia klabu za jinsia, TEHAMA na elimu jumuishi
- Ushirikiano na mrejesho wa wadau umeimarisha utekelezaji
Mikakati ya Kuendeleza Mafanikio ya TESP