Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kuhamasisha watanzania kuendelea kuandika "Maandiko Bunifu" katika nyanja mbalimbali na kutambua kazi hizo kupitia TUZO YA MWALIMU NYERERE ya UANDISHI BUNIFU iliyoanza mwaka 2022.

Mwaka huu 2023 Dirisha la kuwania Tuzo hizo limefunguliwa na nyanja zinazishindaniwa ni Riwaya, Mashairi na Hadithi za watoto.

Fuatilia Mitandao ya Kijamii ya Wizara, Taasisi ya Elimu Tanzania na ya kamati kwa taarifa na maulizo.