Swahili

Chuo cha Ualimu Ilonga kilichopo Kanda ya Mashariki, Kilosa -Morogoro. Chuo hiki kilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1970, kikiwa kinaendesha kozi fupifupi hadi mwaka 1995 serikali ilipokibadilisha na kuanza kutoa mafunzo ya ualimu daraja la A. Serikali pamoja na wadau wengine wa elimu wamefanya jitihada kubwa katika kukiboresha Chuo kwa kuongeza majengo na kuboresha miundo mbinu mbalimbali kwakuwa majengo ya awali yalibinafsishwa kutoka kwa wamisionari. Chuo kimekuwa kikifanya vizuri kitaaluma na katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwa kiwango cha juu.

Category: