[accordion] [acc_item title="Majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni:-"]
- kutunga na Kutekeleza Sera za Elimu, Sayansi, Utafiti, Huduma za Maktaba, Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Uendelezaji wa Mafunzo ya Ufundi;
- kuendeleza Elimumsingi kwa Kutoa Ithibati ya Mafunzo ya Ualimu na Maendeleo ya Kitaalamu ya Walimu;
- kubainisha Vipaji na Kuviendeleza;
- kusimamia Uendelezaji wa Mafunzo katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi;
- kusimamia Mfumo wa Tuzo wa Taifa;
- kuainisha Mahitaji ya Nchi katika Ujuzi na Kuuendeleza;
- kuweka Viwango vya Taaluma ya Ualimu;
- kusimamia Ithibati na Uthibiti wa Shule;
- kusimamia Huduma za Machapisho ya Kielimu;
- kutegemeza/Kuimarisha Utumiaji wa Sayansi, Uhandisi, Teknolojia na Hisabati;
- kuendeleza Wataalamu wa ndani katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu;
- utafiti katika Sayansi na Teknolojia;
- uendelezaji wa Rasilimaliwatu na Uongezaji Tija ya Watumishi walio chini ya Wizara; na
- kuratibu Shughuli za Idara, Mashirika, Wakala, Programu na Miradi iliyo chini ya Wizara.
[/acc_item] [/accordion]