WIZARA YAPOKEA RASIMU YA MABORESHO YA MITAALA ILIYOTOKANA NA MAONI YA WADAU MBALI MBALI

Published on Thursday 02 June, 2022 15:26:54

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Juni 2, 2022 imepokea rasimu  ya maboresho ya mitaala  iliyotokana na maoni ya wadau mbalimbali juu uboreshaji wa mitaala ya elimu nchini ikiwa ni maandalizi ya Kongamano kubwa la siku tatu la kukusanya maoni ya wadau.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka amesema kuwa lengo kubwa la uboreshaji huo wa mitaala ni maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa kwamba mitaala ya elimu ilenge kuwandaa vijana wa Kitanzania wenye ujuzi, uwezo wa kuzalisha mali na kujitegemea baada ya kumaliza ngazi yoyote ya elimu.

Mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma, umewashirikisha Wajumbe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar iliyowakilishwa na Katibu Mkuu Ally Khamis Juma, Ofisi ya Rais TAMISEMI iliyowakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Elimu, Dkt. Charles Msonde.

Washiriki wengine ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Makundi Maalumu iliyowakilishwa na Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Aneth Komba, Kamati ya Kitaifa ya Mitaala iliyowakilishwa na Prof. Makenya Maboko

Read 444 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022