WAZIRI AWAPONGEZA WANANCHI KWA KUJENGA SHULE SHIKIZI.

Published on Wednesday 16 August, 2017 15:14:56

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo ameshiriki zoezi la ufuatiliaji wa miradi ya Elimu Wilayani Kibondo, mkoani Kigoma inayotekelezwa na  Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara yake.Akizungumza katika mkutano na baadhi ya watendaji wa serikali na washirika wa maendeleo waziri  Ndalichako amesisitiza kuwa dhamira ya  serikali ya awamu ya tano ni kuahakikisha Elimu bora inatolewa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya shule.Ndalichako amesema serikali inafarijika sana kuona Wananchi wanajitolea katika kuboresha miundombinu hivyo ameahidi kuchangia mabati 100 ambayo yatasaidi kuboresha ujenzi wa shule shikizi ya Nyamilembi ambayo inajengwa kwa nguvu za  Wananchi."Sisi serikali tunawapongeza sana kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha  Watoto wote wanapata Elimu, na tunapenda sana watoto wote wasome bila kujali maumbile yao, sasa kwa kuwa mmeonyesha dhamira ya dhati ya kujenga shule shikizi na Mimi nitawaunga mkono na ninawaahidi kuwaletea mabati 100"amesema Ndalichako.Waziri Ndalichako amesema Ziara hiyo hiyo pia inalenga kubaini changamoto mbalimbali zinazozikabili shule ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya kibondo Louis Bura amesema kuwa shule shikizi ya Nyamilembi inajengwa na Wananchi kwa kuona na kutambua umuhimu wa Elimu kwa watoto wao.Shule nyingine ambazo ujumbe huo umezitembelea ni pamoja na Shule ya msingi jumuishi  Nengo pamoja na shule ya Sekondari  wasichana KibondoViongozi wengine walioahiriki ziara hiyo ni pamoja na mkuu wa  Wilaya ya kibond Louis Bura, baadhi ya watendaji kutoka Tamisemi,Wizara ya Elimu, wadau wa Elimu, na washirika wa Maendeleo wakiwemo SIDA na DFID.

Read 3749 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022