WATHIBITI UBORA WA SHULE WATAKIWA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU KATIKA MAENEO YAO

Published on Thursday 09 June, 2022 10:11:45

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka amewataka Wathibiti Ubora wa Shule nchini kufuatilia na kusimamia uwajibikaji wa Wakuu wa Shule kwenye  fedha za miradi ya ujenzi wa shule zilizopelekwa na Serikali katika maeneo yao.

Amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa kufunga kikaokazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara.

Amesema kuna ujenzi wa miundombinu ya shule unaendelea ikiwemo kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambapo amewataka kuhakikisha wanashiriki usimamizi wake na kutoa ushauri katika kuzingatia vigezo vya ubora vinavyohitajika  kulingana na miongozo na Sera.

Aidha, amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza majukumu Wathibiti Ubora kwa kuongeza eneo la Uthibiti na  ufuatiliaji kwa Vyuo vya Kati na Ufundi (VETA) ambavyo vinatarajiwa kuwepo katika kila Wilaya ifikapo mwaka 2025.

Amesema wathibiti ubora wa shule wanaweza kuisaidia Serikali katika kuhakikisha elimu bora yenye kuwasaidia vijana kupata maarifa, stadi na ujuzi inapatikana kwa kukagua vyema shule na vyuo vya ualimu.

Sedoyeka ameongeza kuwa Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika idara hiyo ikitambua kuwa wathibiti ubora ni mboni ya jicho ya elimu na amewahimiza wakasimamie ubora wa elimu kwa kuwa matokeo ya uthibiti ubora ni kuwepo kwa elimu bora huku akisisitiza suala la kuzingatia matumizi ya TEHAMAkatika utendaji.

"Ni wakati muafaka kufikiria ni namna gani mnaweza kuzifikia shule hata bila kufika physically ili kufanya ufuatiliaji," amesema Prof. Sedoyeka.

Kwa upande, Mkurugenzi Msaidizi Uthibiti Ubora upande wa Ualimu, Mathias Mvula amemweleza Katibu Mkuu kuwa kikao hicho kimekuwa na tija kwa kuwa wamepata fursa ya kufanya tafakari ya pamoja kuona yale waliyoyapanga kama yametekelezeka na kupanga mikakati ya utendaji ili kuongeza ufanisi.

Akizungumza kwa niaba ya Wathibiti ubora hao,  Amon Lembao kutoka Kanda ya Kati, amemshukuru Katibu Mkuu Sedoyeka kwa kuwezesha kikao hicho kwa kuwa mada zilizotolewa zimewapatia mahiri mbalimbali zitakazokwenda kuwasaidia katika utendaji.

Read 299 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022